MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amejikuta akitafunwa na skendo ya uchawi kutoka kwa watu wake wa karibu ambao alikuwa anaishi nao, New Delhi nchini India, kutokana na mambo yake kumuendea poa huku wenzake yakibuma. Chanzo chetu kutoka nchini humo kilidai kuwa, wasichana wengi wa Kibongo waishio India wamefurahi mno kusikia msanii huyo kafungiwa na Naibu Waziri, Juliana Shonza kufanya sanaa, sababu alikuwa anawatambia mno. “Pretty kwa Wabongo wengi kule India wanamjua kwa kutumia ‘ndumba’ ili mambo yake yamnyookee kwani alipokuwa huko alikuwa akiwazidi wasichana wote na kila alichokifanya kilikuwa kikimnyookea tofauti na wengine. “Hali hiyo ilisababisha minong’ono sana mpaka ameondoka na hakuna aliyempenda,” kilidai chanzo hicho ambacho kiliomba kuhifadhiwa. Badaa ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilimsaka Pretty ambaye alifunguka kama ifuatavyo: “Jamani mimi siyo mchawi, wananizushia sababu ya chuki zao binafsi, mimi nipo karibu na Mungu kuliko wanavyodhani, hata usiku huwa nakesha nikisali, sasa huo uchawi nafanya saa ngapi.”