Mabingwa wa tetezi Tanzania bara klabu ya  Yanga kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten, imesema imedhamiria kuiandikia barua Bodi ya ligi kuomba kusogezwa mbele kwa mchezo wake  wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ten ameweka wazi hilo huku akitaja sababu kubwa kuwa ni ugumu wa ratiba unaoikabiri timu hiyo hivyo inahitaji kupata muda wa maandalizi ya mechi ya Ligi ya mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana utakao pigwa tarehe 06 mwezi wa tatu mwaka huu na mechi ya marudiano ikipigwa tarehe 16 mwezi wa 3 pia.
”Tunatazama uwezekano wa kupeleka barua kwenye shirikisho au bodi ya ligi ili kuomba mechi yetu dhidi ya Mtibwa isogezwe mbele tuweze kujiandaa vizuri na mechi ya kimataifa, tunataka kushinda ili tufike mbali zaidi ya tulipoishia msimu uliopita”, amesema.
Yanga imeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Songea kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho dhidi ya Majimaji na baada ya mchezo huo itaelekea Mtwara kucheza mchezo wa ligi na Ndanda FC Februari 28 kabla ya kurejea na kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Machi 3.