Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Zahir Ally Zorro amesema anaamini serikali itafanishwa kukamatwa kwa aliyesababisha kifo cha Mwanafunzi Akwelina Akwilini ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano.

Zahir Zorro ambaye ni baba mzazi wa wanamuziki Banana na Maunda Zorro, ametumia mtandao wa twitter kuipongeza serikali kwa kugharamikia mazishi ya Akwelina na kutoa rai hiyo.

“Ahsante kwa Serikali yetu Sikivu. Kusikia kilio cha wengi na kujitoa kumrudisha Akwilina Nyumbani, vifo hutokea kwa wakati na muda uliopangwa, japo sababu hutatanisha. Tunaamini Mkono Mrefu wa Serikali utafanikisha kukamatwa Muuwaji. Ni vyema akamatwe au Atauwa tena tu!,” amesema Zahir Zorro.

Marehemu Akwelina Akwilini ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha NIT aliuawa kwa kupigwa risasi February 16 mwaka huu katika maandamano yaliyojumuisha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). mwali wa Akwelina ulizikwa hapo jana katika kijiji cha Kitowo kata ya Marangu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.