MY AMERICAN EXPERIENCE” Wakati ninapigana namna ya kumrudisha mke wangu maisha mengine yalikua yanaendelea kama kawaida napiga kazi na ninaenda Shule Jioni huku ninalea mtoto wangu wa kiume thanks God for the House Girl alikua ni msichana muelewa sana lakini Wabongo pale USA pamoja na majirani wa mke wangu Bongo wakaanza kunizushia kua nimemgeuza kua mke wangu it was fun on my part nilikua nacheka kimoyo moyo maana it was a big joke of my life nianze kutembea na House Girl kwa kawaida hua ninaogopa sana ku take advantage of the helpless …Shuleni kama kawaida this time nilikua nimekutana na somo la Politics my fav na hii ni kwa sababu nia na madhumuni yangu ya kusoma Sheria yalikwama kutokana na malipo kua makubwa sana so nikaamua Political Science will do nikakutana na “FOUNDING FATHERS OF AMERICA: na nikakutana na “THE USA CONSTITUTION” halafu “THE SEPARATION OF POWER” pia “THE SUPREME COURT OF USA” ..”THE CONGRESS” na “THE EXECUTIVE BRANCH” humu mote I was at home lakini in the end ukaja mtihani maalum ambao ni Sheria kwamba ni lazima ufanye huo mtihani ambao hauhusiani na darasa kabisa ni mtihani unao base kwenye English kuhakikiaha unamaliza ukiwa unajua English walioupanga wanajua kua kuushindwa ni kitu rahisi sana so unaruhusiwa kurudia mara 3 ukishindwa zote ni sawa hukusoma kabisa unatakiwa kurudi kuanza zero tena …nilishinda mara ya kwanza tena kama mchezo nikapata my BA in Political Science .kazini nikaomba kuanza kwenda masafa marefu kwa hiyo nikaanza safari za loong distance from New York to Florida na nikaanza kupiga USA nzima sijafika Alaska tu nimefika States zote zingine na hata leo ukinipeleka ninaweza kukufikisha popote pale bila tatizo bado ninakumbuka safari yangu ya kwanza to Salt Lake/Utah State Jimbo ambalo mpaka leo mweusi ni kichekesho kwa wazungu I mean kuendesha masafa marefu it was fun ila Sheria zake ni kali sana na hasa ya masaa ya kuendesha unaruhusiwa Masaa 11 tu inapofikia hapo hapo unasimama unalala kwa masaa 10 unapokua safarini kule Ofisini wanaku monitor na wanajua kila ulipo na infact wanajua mpaka speed yako ukiwa unakimbia sana wanakupigia simu kua punguza..njiani nilikua nahangaika na simu Bongo!.ITAENDELEA