Mlinzi wa AS Roma Aleksandar Kolarov ameeleza kuchukizwa kwake na kauli chafu zenye vimelea vya laana zilizotolewa na kocha was AC Milan Gattuso na kumuelekea yeye.

Kolarov amesema kuwa wakati akijiandaa kurusha mpira alianza kubuguziwa na Gattuso kwa maneno ya kejeli ambayo hakutaraji kutoka kwenye kinywa cha kocha huyo.

“Alinifuata huku akiniambia kuwa Nina bahati sikucheza soka kipindi ambacho yeye alikuwa uwanjani, kwa maana kipindi chake hakukuwa na warembo kama Mimi wenye maumbile ya kuvutia na kutia hamasa”.

Milan iliibuka na ushindi wa kibabe wa goli 2-0 kwenye Dimba LA Olympico jijini Roma.

Match photo