STAA mwenye kuijulia mitindo ya nguo Bongo, Jacqueline Wolper anajutia kupoteza muda wake mwingi kukomaa na filamu, badala yake anaona ni bora tu angeanza biashara yake ya ushonaji wa nguo anayoifanya kwa sasa.

Wolper aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, miaka 10 iliyopita alitumia nguvu kubwa mno kukuza jina lake kupitia sanaa, lakini ukweli ni kwamba angetumia nguvu hiyo kukuza kipaji chake cha ushonaji leo angukuwa bonge moja la tajiri Bongo.

“Ningejua tangu mwanzo ningekomaa na mitindo maana huku naona watu wananielewa na ninapata pesa nyingi, lakini kwenye filamu nimeishia kujulikana tu,” alisema Wolper.