Nyota Mbrazil, Neymar akiugulia maumivu Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris dakika ya 80 jana kabla ya kutolewa kwa machela timu yake, PSG ikishinda 3-0 dhidi ya Marseille katika mchezo wa Ligue A, Ufaransa mabao ya Kylian Mbappe dakika ya 10, Rolando aliyejifunga dakika ya 27 na Edinson Cavanidakika ya 55.

Neymar sasa yuko shakani kucheza mechi ya marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mjini Paris baada ya kufungwa 3-1 Februari 14 mjini Madrid