Vinara wa ligi kuu Tanzania bara wekundu wa msimbazi Simba watashuka dimbani hii leo kuvaana Mbao Fc kutoka jijini Mwanza. Simba ambao wanatakribani point 42, watakua wenyeji wa mchezo huo utakao chezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia hali ya nahodha (John Bocco) wa klabu hiyo, daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema Bocco yupo fiti kucheza mchezo wa leo endapo kocha akimuhitaji. “Bocco yupo fiti, yalikuwa ni majeraha madogo sio yakumkalisha nje mda mrefu na tiba zilikwenda sawa na yupo fiti”, alisema.

Bocco aliumia kwenye mpambano kati ya Simba na Mwadui Fc uliochezwa huko Shinyanga na kumalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma alijitamba kwa kusema kuwa wameandaa kikosi chao kwa ajili ya kupata ushindi na aliendelea kusema kuwa kikosi chao kipo kamili na wanatambua kuwa Mbao ni timu nzuri lakini wao wamejipanga kwa point tatu muhimu.

Kocha wa Mbao Fc Etienne Ndayiragije, amesema waowamefata point tatu Dar es Salaam na wanaamini pointi hizo zitapatikana na sivinginevyo.

Image result for simba sc vs mbao fc

Pambano la raundi ya kwanza lililopigiwa katika dimba la CCM Kirumba Mwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana goli mbili kwa mbili.

Image result for simba sc vs mbao fc