Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amewapongeza viongozi wa chama cha soka mkoani Kigoma kwa kufanikisha ujenzi wa ofisi za kisasa za chama hicho.
Mwakyembe amezitoa pongezi hizo leo wakati akifunga kozi ya makocha wa ‘Grassroots’ kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12 Wasichana na Wavulana kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Ujiji, Kigoma.

”Nitumie nafasi hii kuwapongeza viongozi wote wa chama cha soka Kigoma kwa kutengeneza ofisi nzuri za chama chenu kwa viwango vya kisasa, mikoa mingine muige hapqa, tunawenyekiti wa Tabora, Katavi na Mara pitieni muone ofisi ya wenzenu”, amesema.

Mbali na kufunbga kozi hiyo Mwakyembe pia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ufunguzi wa Ligi Kuu ya soka ya Wanawake Tanzania ambao utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz dhidi ya Simba Queens.