MY AMERICAN EXPERIENCE” Picha hii nilikua Hospitali wakati anazaliwa mtoto wangu wa kike New Rochelle/New York…nikiwa ninapigana na maumivu ya kuelekea Divorce siku moja kikaja kishindo kazini Joe Orlando Owner aliniita ofisini kwake akaniambia Serikali imemlazimisha auze kampuni na kwamba hawatampa tena kibali cha kuendelea nayo kwa sababu wanaamini yeye ni member wa Mafia Mob na kwamba tayari ameshapatikana mnunuzi kampuni ya Sterly Circle Harzadous Inc. akaniambia ukweli kwamba kampuni hiyo imeshasema itapunguza watu wengi sana watachukua watu 10 tu wao wanayo mnapower ya kutosha wanahitaji watu 6 kutoka management na Madreva 4 tu akaniambia the Good news mimi ni mmoja wa 4 hao lakini akaniambia Kampuni mpya wameshitushwa sana na masaa yangu ya kazi kua ni mengi mno so hawataniruhusu tena kuwa na hayo masaa …baada ya kumaliza Degree ya Political Science nilijaribu kutafuta kazi ya Ofisini sasa tabia ya USA ukiomba kazi wanakuuliza mshahara unaopata unapofanya kazi nilikua ninapata Dola 25 kwa Saa moja ni mshahara mkubwa sana wakawa wananishangaa kua sio rahisi kupata kazi ya kuzidi huo mshahara so nikawa ninaendelea kupiga kazi ya kusukuma 18 Wheeler toka nipate Leseni ya CDL Class A nilikua sijawahi kupata Mshahara wa halali wa masaa 40 kama Sheria ya USA inavyotaka nilichokua ninakijua ni Mshahara mkubwa wenye Overtime nikajiaminisha kua Mshahara wangu ni kati ya Dola 2000 mpaka 3000 kwa Wiki kumbe nilikua ninajidanganya sana baada ya kampuni kuuzwa waajri wapya wakanibana nikawa nafanya kazi msaa 40 tu kwa Wiki kwa mara ya kwanza nikapata mshahara wangu wa halali ambao baada ya makato uliishia kua Dola 700 tu!..I was in a Shock sikuamini cause no way ninaweza kuishi kwa ule mshahara maisha yangu yalishavuka level ya Dola 700 ninaanzaje kurudi nyuma? I was living large magari 3 ya kisasa BMW. Acura Legend na Nissan Pathfinder mpya kabisa with zero Milage nyumba kubwa 3 bedrooms na upande wa pili Divorce inaita kwanza nikaamua kutafuta nyumba ya One bedroom nikahama pale Nikaachana na magari 2 USA sio rahisi kuuza gari ulilokwisha litumia so ukilichoka unawapa Charity NGOs wanakupa fomu maalum mwisho wa Mwaka unaomba tax returns ..ITAENDELEA!

SHARE
Previous article
Next article