Msanii wa muziki, G Nako amesema wasanii wa Bongo kufanya kolabo na wasanii wa kimaitafa ni kitu kirahisi ila kuna vitu vya kuzingatia.

Rapper huyo kutoka kundi la Weusi ameiambia kuwa kolabo za kimataifa wao kama Weusi wameshafanya ili kinachoangaliwa ni namna ya kuzitangaza.
“Lengo hasa la kufanya kolabo lazima iwe watu wawili na ionekane kwamba lazima pande zote mbili zinanufaika, ninapofanya kolabo na wewe natarajia ufanye promotion katika nchi yako na mimi hali kadhalika nifanye promotion kwenye nchi yangu,” amesema G Nako.
Moja ya kolabo kubwa kutoka kundi la Weusi ni pale walipowashirikisha Collo, Rabbit na Nazizi kutoka nchini Kenya na Navio kutoka Uganda katika remix ya ngoma yao inayokwenda kwa jina la Gere