KUTOKANA na gumzo ambalo linaendelea kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii, juu ya mtu aliyemtundika ujauzito mwanadada Dayna Nyange, kuzidi kushika kasi, mwenyewe ameibuka na kutoa la moyoni.

Akichonga na Full Shangwe, Dayna aliyetoa Wimbo wa Sale Sale, alisema kuwa, watu kubashiri mara kwa mara juu ya baba wa kijacho wake ni kwa sababu wana hamu sana ya kumfahamu na kiu yao anakwenda kuikata hivi karibuni.

“Muda si mrefu ninakwenda kumtambulisha baba kijacho wangu, nakwenda kufanya hili kwa sababu watu wanaonekana wana kiu sana ya kumfahamu kiasi kwamba wanakuwa wanabashiri mpaka kuwagusa wasionihusu kabisa,” alisema Dayna.

Alipoulizwa lini hasa anakwenda kufanya hivyo alisema ni surprise lakini ni katika kipindi kifupi kuanzia sasa!