Msanii Edu Boy amedai kuna taarifa kuwa Stamina anamtafuta ili kumpiga baada ya kumchana kwenye ngoma yake ‘Tunasafisha’ ila ni kitu ambacho hakimuumizi kichwa.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa haishi kwa sheria za mtu yeyote na iwepo Stamina anamtafuta yeye sehemu yoyote anapatikana.

“Siishi chini ya sheria ya mtu, naishi chini ya sheria za nchi ila siishi kwamba nikimchana Stamina nitakutana naye anipige, kwanza hana uwezo wa kukutana na mimi anipige naamini kwa asilimia mia,” amesema.

Ameongeza kuwa anajua fika kwa sasa wasanii wengi hawampendi kutokana amekuwa na tabia ya kuwachana kila mara ila jambo hilo halitomzuia kufanya muziki wake.