Miongoni mwa watoto wa mastaa Bongo wenye kukodolewa macho zaidi mtandaoni kwa sasa, ni mtoto wa waigizaji Ray Kigosi na Chuchu Hansy ‘Jaden’.

Umaarufu wa wazazi wake umemfanya na Jaden kuwa maarufu pia kitu kinachofanya wengi kumjua na kumfuatilia sana.
Umaarufu wa Jaden haujaishia kukodolewa macho na mashabiki wa wazazi wake pamoja na waandishi wa habari za kidaku katika mitandao na magazeti.
Umaarufu wake umevuka mipaka na kufanya kukodolewa macho na kampuni mbali mbali zikitaka kumtumia katika kutangaza huduma/bidhaa zao.
Kwa sasa Jaden ana dili kadhaa ikiwemo kutoka Bank ya NMB na duka la Robby One Fashion. Jaden anaungana na watoto wasanii wengine kama Tiffah wa Diamond na Gold wa Navy Kenzo ambao ambao ni mabalozi wa kampuni mbali mbali.
Kwa sasa Jaden ana followers 107k katika mtandao wa Instagram akiwafukuzia na kina Tiffah, followers Milioni 1.6 na Nillan, followers 543k (wote wa Diamond, pia kuna Cookie wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo, followers 420k.