Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee amesema kuna kitu atafanya na msanii wa Uganda, Weasel mara baada ya kifo cha Mowzey Radio aliyekuwa akiunda kundi la GoodLyfe na Weasel.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Kisela’  kuwa kabla ya kifo cha Mowzey Radio kuna video walikuwa waka-shoot kitu ambacho kilishindikana.
“Before amefariki Radio tulikuwa tunaenda ku-shoot, tulikuwa na script kila kitu tayari, in fact nilikuwa nimeshaweka deposit ya video lakini imetokea ilivyotokea,” amesema Vanessa.
“Lakini Weasel nazungumza naye kila siku na tujianda kufanya kitu so special kwa ajili ya mashabiki zake na familia yake kuenzi kazi yake,” amesisitiza.
Ameongeza kuwa Mowzey Radio alipopata ajali Weasel alimtumia ujumbe kuwa akamuone lakini alishindwa kwa sababu ndio alikuwa ametua Lagos, Nigeria, hata hivyo alipanga baada ya kumaliza tour Lagos angeenda Uganda.