Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’ amefunguka na kurusha jiwe gizani kwa kusema hakuna kitu ambacho anaweza kuwalipa watu waliomtendea mema na hata mabaya mpaka kufikia sasa alipo.
Barnaba ametoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake maalumu wa kijamii mchana wa leo baada ya kile kinachodaiwa na watu wengi huenda maneno hayo aliyoyatoa bado yanamlenga mzazi mwenzake mama Steve ‘Zuu Namela’ kutokana na kutengana kwako huku wengine wakidai huenda ni mashairi ya wimbo uliopo katika albamu yake anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

“Ukimtumainia yeye kila kitu kitaenda sawa tumpe sifa na utukufu Mungu wetu aliyejuu ‘major day’ na tujifunze kusamehe haraka na kutoa tulivyonavyo moyoni ili tuwe na nafasi kubwa kwenye milango ya mbingu. Hakuna kitu naweza kulipa kwa mlionitendea mema na kwa watenda mabaya, zaidi ya Mungu pekee. Mimi ni mwenye kutambua thamani ya kila aliyepandikiza nguvu ndani ya kipaji changu ‘so’ sina budi kusema asante mungu kwa kuniweka adi Leo”, amesema Barnaba.

Kwa upande mwingine, msanii Barnaba amesema anajisifu kwa sauti yake ambayo kwa sasa imekua sehemu ya burudani au nusu chakula juu ya muziki wake.