Msanii wa muziki Bongo, Mimi Mars amesema ngoma yake ‘Sitamani’ ndio ngoma iliyompa changamoto katika kurekodi tangu alipoanza muziki.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa katika ngoma hiyo alilazimika kuimba kwa sauti ya juu zaidi tofauti na ngoma zake za awali.
“Katika ngoma zangu tatu ambazo nimezitoa, ngoma iliyonipa stress au ugumu zaidi ni Sitamani kwa sababu ilibidi nipangilie sauti yangu katika kiwango cha juu zaidi kuliko nilivyozoea kwenye Sugar na Dede kwa hiyo ni kitu ambacho nilikuwa najaribu kipya,” Mimi Mars ameiambia Clouds Tv.
Mimi Mars ambaye anafanyakazi zake chini ya Mdee Music hadi sasa ameshatoa ngoma tatu ambazo ni Dede, Sugar na Sitamani iliyofanyika Switch Music Group na producer S2kizzy.