Mastaa kupitia mitandao ya kijamii imekuwa ni kitu cha kawaida kwao kufanya hivyo ambapo hutumia mitandao yao kutaniana  na hivyo  mashabiki huona kama ni kitu cha kawaida kwa mastaa kufanya hivyo
Kupitia mtandao wa instagram wa staa wa muziki wa Hip Hop Nikk Wa Pili ame-post picha ya mpenzi wake na kuandika ujumbe ambao wengi wameutafsiri tofauti akiwemo Dogo Janja ambaye ame-comment na kufanya utani juu ya kile ambacho Nikk Wa Piliamekiandika kuhusu mpenzi wake.
Nikk Wa Pili ameandika “Kuwa mzuri hakuitaji shoping ya Dubai, wigi la malaki, make-up sijui ya saloon gani, wala kamera na maediting kuwa mzuri ni kuwa wewe Sunday swagg picha by me”