Manchester United wamepoteza mchezo 1 tu kati ya 9 ya klabu bingwa Ulaya waliocheza nyumbani dhidi ya timu kutoka nchini Hispania huku wakishinda mechi 5 na kutoa sare 3, Mara ya mwisho kupoteza nyumbani dhidi ya timu kutoka Hispania ilikuwa msimu wa 2012/13 walipofungwa 2-1 dhidi ya Real Madrid kwenye hatua kama hii ya 16 bora.

Leo wanaingia uwanjani kucheza na Sevilla ambao kwenye mechi 4 ya UEFA walizoenda kucheza kwenye Ardhi ya Uingereza hajawahi kushinda mchezo wowote, wamefungwa mechi 3 na kutoa sare 1.
Mechi ya kwanza iliisha 0-0, Leo hali itakuwaje?