Nyota wa zamani wa majogoo wa jiji la Liverpool na Mchambuzi wa Soka katika kituo cha Sky Sports, Jammie Carragher, amesimamishwa kazi kwa muda kwa kitendo cha kumtemea mate binti ambaye ni shabiki wa Manchester United.

Carragher alifanya tukio hilo mapema baada ya mchezo uliowakutanisha Manchester United dhidi ya Liverpool wakati akitoka kukava habari kuhusiana na mchezo huo.

Kwa mujibu wa Sky Sports TV, Msemaji wa kituo hicho amesema Carragher hatokuwepo kazini kwa takribani wiki moja inayokuja, na baadaye watakuja kutoa hatma ya mchezaji huyo kama ataendelea kusalia kazini au kuondoshwa kabisa.

Kufuatia kitendo hico, Carragher tayari alikuwa ameshaomba msamaha kwa binti huyo mwenye miaka 14 na msamaha wake ulipokelewa.