Mkuu wa mkoa  wa Mbeya  Leo  amefanya ziara wilayani Kyela  amekagua  ujenzi wa barabara ya  KIKUSYA – IPINDA – MATEMA  inayojengwa kwa kiwango cha lami  yenye urefu  wa 34 Km  na inagharimu shilingi Bilioni 56.9 

– Akiwa ktk mikutano ya hadhara  nyakati  tofauti  leo ktk kata ya MATEMA  na IPINDA  Amesema  kukamilika kwa barabara hiyo  kutachochea  biashara ya mazao,  uvuvi  na utalii
–  Aidha  ametembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya IPINDA  ambako  Ameupongeza uongozi wa halmashauri,  Kamati ya UJENZI  na wananchi kwa kutumia vizuri fedha sh milioni 500 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya UJENZI na ukarabati

Amesema  kituo cha IPINDA ni cha mfano  na amewaomba wananchi waendelee  kushirikiana na serikali  kujenga  pia zahanati ktk vijiji