Msanii wa filamu Bongo, Steve Nyerere amesema tasnia hiyo kwa sasa inaongoza Afrika Mashariki na Magharibi kwa kutoa tamthilia zenye ubora.
Muigizaji huyo  kuwa mafanikio hayo yamefikiwa baada ya wasanii kugundua sehemu waliyojikwaa na kuamua kuinuka na kuanza upya.
“Tumesimama sasa katika Afrika Mashariki na Magharibi yote tunaongoza kwa kuonyesha tamthilia zenye ubora, inaonyesha ni kwa kiasi gani Tanzania kuna vipaji,” amesema.
Ameongeza kuwa kilichobaki kwa sasa ni wasanii kuongeza thamani ya kazi zao na kujithamini na sio kuwa kawaida kwenye kila jambo ambalo wanafanya.