Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard Wambura, ameimgia matatani kwa tuhuma za kupokea pesa kinyume na taratibu za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine ya kinidhamu.
Wambura amefikishwa mbele ya Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ambayo inakutana leo Jumatano Machi 14, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala lake.
Makosa matatu ya Wambura yatakayojadiliwa na kamati leo ni kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.
Wambura ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye soka la Tanzania ikiwemo klabu ya Simba na Chama cha soka mkoa wa Mara, alichaguliwa kuwa makamu wa Rais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Dodoma mwaka jana.