Wahaidi  kuleta wanafunzi madaktari mkoa wa Mbeya
– Wahaidi  kuongeza fedha kwa ajili ya MAPAMBANO DHIDI YA ukimwi
Mkuu  wa mkoa wa Mbeya  Leo amekuwa na mazungumzo   na uongozi wa Henry  Jackson  Foundation (HJF) ya MAREKANI  pamoja na mambo mengine ujumbe wa HJF ukiongozwa  na Rais  Joseph Caravalho  amehaidi kuwa taasisi yake itaongeza   fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukimwi ktk mkoa wa mbeya

Katika miaka miwili HJF imetumia dola milioni 14 ktk kampeni  ya mapambano  ya ukimwi mkoa wa Mbeya  kwa kuzisaidia taasisi  mbalimbali  zinazojihusisha na mapambano ya ukimwi
Aidha amehaidi kupitia  taasisi hiyo italeta  wanafunzi madaktari wafanye  kazi kwa vitendo ktk hospitali na vituo vya Afya mkoa wa Mbeya

Mkuu wa mkoa ameshukuru serikali ya MAREKANI kupitia taasisi hiyo kwa misaada mingi ikiwemo UTOAJI elimu  , vifaa na uwekaji wa umeme   wa jua ktk baadhi YA vituo vya Afya
Amewahakikishia usalama kwa wanafunzi madaktari  watakaokuja  mkoani mbeya  kutoa huduma ya afya