Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, amemtabiria mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa Aslay kwamba ni kijana atakayekuja kuwa nyota mkubwa sana kutokana na kazi zake jinsi anavyozifanya.
Mh. Kingu amesema kwamba anamkubali sana mwanamuziki huyo kwa sababu  ya hekima zake na anaishi maisha ambayo yako simple sana.
Aidha Mbunge huyo amekiri kuwa ipo siku atamtafuta msanii huyo ili aweze kumpatia sifa zake na kumpongeza juu ya wimbo alioufanya na mwanadada Nandy ‘Subalkher’.
Mbali na Aslay, Mbunge huyo kijana amesema anamkubali sana mwanamuziki Cyrill Kamikaze ambaye anauwakilisha vizuri mkoa wa Singida, Chegge kutoka TMK, pamoja na Angel Bernad anayeimba nyimbo za injili.