KUTOKANA na hivi karibuni kufungiwa kujihusisha na sanaa kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kujiachia nusu utupu mitandaoni, msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amemwangukia waziri huyo kwani mambo yanamwendea kombo.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kuwa, kwa sasa yupo kwenye harakati za kuandika barua kwa Waziri Shonza kwa ajili ya kumuomba msamaha, angalau ampunguzie adhabu kwa kuwa amekuwa hohehahe asiyejielewa afanye nini.
“Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa naibu waziri maana maisha hayaendi,”  alisema Pretty Kind.