MKALI wa michano, George Mdemu ‘G Nako’, amefunguka kwamba siku za hivi karibuni amekuwa akiwaona wakongwe na mastaa wengi wakifunga pingu za maisha jambo ambalo limemvutia na yeye kufikiria kuoa.
Akipiga stori na Risasi Vibes, G Nako alisema kwamba kutokana na kuvutiwa huko na yeye yupo kwenye maandalizi na siku si nyingi atafunga pingu za maisha na mpenzi wake ambaye kwa ambao hawam-fahamu siku ya ndoa yake ndiyo atamtambulisha rasmi.
“Nafikiria sasa kuoa. Umri ndiyo huu na nimevutiwa na mastaa wengine ambao wameweza kuvuta majiko yao. Kwa hiyo hata mimi nitajitosa hivi karibuni,” alisema G Nako.