Wastara amesema hayo alipokuwa KIKAANGONI Wastara anasema kuwa alimuandikia barua Diamond Platnumz kuomba msaada pamoja na Alikiba lakini kwa Diamond alionekana yeye ni kama tapeli.”Niliandika barua kuomba msaada hivyo nilimuandikia Diamond lakini watu wake walimfikishia taarifa kuwa mimi tapeli hivyo hakuweza nisaidia ila pia wakati huo huo nilimuandikia Alikiba na Alikiba akaniambia kuwa kuna watu walikuwa na show yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye anazohitaji hivyo akaniahidi kuwa atakwenda kufanya show hiyo ili aje kunisaidia, kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo” alisema Wastara.
Mbali na hilo Wastara amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.

Aibua mapya kuhusu Mange Kimambi

Msanii wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo maana anakurupuka katika baadhi ya mambo.

Wastara amesema hayo  na kusema kuwa Mange Kimambi alizusha juu ya Cannula aliyowekwa mkononi na kusema alijiwekea mwenyewe, Wastara amesema kuwa mbali na kuzusha huko lakini dada huyo alikwenda mbali mpaka kuwauliza madaktari wa hospitali aliyokuwepo kama anatibiwa hapo.”Mange Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe” alisema Wastara
Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha.