PART 20: “MY BONGO EXPERIENCE” Becoming Akili Kubwazz ni a process na hasa ya kuweza kutafakari na kujua na kukubali ukweli bila kulazimishwa wala kuambiwa ni moja ya tatizo namba moja linalowatesa Wabongo wengi wanaoenda Majuu na kurudi Bongo ni kwamba kumbe unapoishi Majuu kwa muda mrefu una develop tabia mpya nyingi bila kujua kwa mfano Majuu maji au umeme havikatiki hata siku moja so umezoea kuwa ni guarantee vipo now unarudi Bongo kukatika ni kawaida kama hukutuliza akili utaanza wazo la kurudi Majuu yote yalinikuta lakini dhamira ya kuishi bongo ilikua inanisuta kuvumilia ..at this point nilikua nam date Mwanasheria mwanafunzi she was a fine lady with class ila bado mabadiliko ya mfumo wa Mwanaume kulipia kila kitu kwenye maisha ya mapenzi ya Bongo ilikua inanipa taabu kidogo I mean Majuu Mbebezz analipia pia infact inakua ni kama zamu leo Mamen na kesho Mwanamke mnasaidiana bila Vita wala Ugomvi na wote mnafanya kazi so hakuna muda wa kufuatana fuatana mpaka mwisho wa wiki ndio mnakutana full …Bongo Mwanaume unatakiwa kulipia kila kitu Mwanamke hata akiwa nazo hatoi now tatizo ni zikikuishia ina maana na mapenzi hamna tena now sikujua kwamba na upole wote aliokua nao my Date na yeye alikua anapenda pesa zaidi until one day nilipokuja kugundua the Ugly truth kwamba alikua akitegemea pesa kutoka kwangu zaidi lakini hakua na mapenzi kama alivyokua anaigiza so kama kawa nilipogundua the truth nikaachana naye na nikaanza na Miss IFM ambaye kwa mara ya kwanza nikawa nimekutana na Mbebez tofauti sana hakuwa motivated na pesa on a serious note alikua anasoma na anafanya kazi kama nilivyokua ninaishi Majuu I was shocked na pia very impressed but nikagundua kuwa she was so naive that nikijiachia kumpenda siku akiamka nitaumia so I was so careful kutoachia my guards …on the other hand biashara yangu ya Social Media was on fire pole pole Wabongo walikua wameanza kuelewa umuhimu wa Social Media so matangazo yalikua mengi na tayari nilikua ninafanya kazi na makampuni mengi makubwa na pia nikaanza mpaka kusafiri nje ya nchi kupiga kazi miaka 2 tu baada ya kuanzisha kampuni yangu ya “BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD” mara ya kwanza nilienda Accra/Ghana…ITENDELEA