BINTI anayefanya vizuri kwenye Bongo-fleva, Nandy alishafunguka kipindi cha nyuma kuwa kama kutoa penzi ni bora kwa mwanamuziki mwenzake, Billnas na sio Dogo Janja kama wanavyosema watu.

Leo Picha za wawili hao zimevuja kwenye mitandao ya kijamii wakiwa pamoja huku mashabiki wao wakishangilia kuwaona wakiwa wote na wamewapongeza kuwa waendelee kuwa pamoja.

Mashabiki walienda mbali kwa kusema wanapenda kuona ndoa ya wasanii hao.