“Jana ilikuwa Siku Yangu Nzuri Ya Kumbukumbu na Siku Ya Kuzaliwa Kwangu,

Siku Moja Nyuma alinitafuta Nandy ambae tuliwahi kuwa kwenye Mahusiano Ya Pamoja kwa kipindi, akaniomba nimtumie picha zangu na yeye za Pamoja a post kwajili ya Birthday Yangu nikamueleza ukweli Sina Memory yeyote ya pamoja na Wewe Sababu tulivyoachana nilifuta na Naheshim Mahusiano niliyonayo Sasa ! Kwa Bahati Mbaya nilichelewa Kuamka Jana nikakuta sim Nyingi za Interviews I thought ni kwajili ya Birthday Wishes.

Then nikakutana na interview zinazotaka nieleze juu ya picha iliopostiwa na Nandy,Sikuwa na jibu Sababu sie niliepost na sikuwa nayo hata kwenye backup hizo picha nikafuatilia nikakuta picha imepostiwa na @reyjons na @officialnandy mwenyewe! Nikamtafuta Reyjons kwa WhatsApp kwanini umepost vile ?madhara yake si unayajuwa….akaniambia ametumwa na Nandy Mwenyewe,then ikapostiwa na Nai Official Ambae ni rafiki wa Nandy !ikaniletea Shida sana kwa Mpenzi wangu nilijitahidi kujielezea lakini Swali lilikuja hata kama mmeachana anapata hiyo authority ya kupost ??ikabidi nimtafute Nandy na kuhoji kwanini upost picha kama Ile?? Akasema ni Gift yako ya Birthday nimetaka utrend! Sikuelewa nikamuuliza umetazama upande wangu lakini ??akatuma Voice Notes ambayo ninayo akielezea kwanini kapost ile picha na Mipango ya utoaji wake wa Wimbo Mpya !

Uzuri Nina hyo Voice notes na Baadhi ya sms sababu Mawasiliano tulikuwa tunafanya Snapchat !kwa kinywa Chake Mwenyewe alinieleza wamepanga kick kubwa na team yake itanihusisha mimi nikahoji Sana ni kick gani hyo ?nimpige ASLAY kwenye video yake kwa Utani !

Hakujibu tena text leo nimeamka kama Saa 8 au Saa 9 Mchana maaana nililala Saa 2 asubuhi ! Nilivyoamka Nimekuta sim Nyingi Za Ndugu,Jamaa,Watangazaji na Marafiki lakini nilikuwa nashindwa kupokea Sababu ya tatizo la WhatsApp Call Hapa UAE, nikabahatika Kuiona hyo VIDEO kiukweli Nimelia Sana, Hakuna kitu kinaniuma Kama Mama Yangu Mzazi anavyonipenda akutane na tukio kama hili…Nikajaribu Kumtafuta Manager wangu Mchafu afanye Mawasiliano na Nandy kuona imekaaaje lakini Nandy alisema hajui lolote na aliwahi kunitumia hii VIDEO kitu Ambacho sio Kweli hata kidogo ,Niko na Akili zangu Timamu

Niko na Akili zangu Timamu Nasema kama kuna njia yeyote aliwahi kunitumia video hyo ama kwa WhatsApp au popote niko teyari kuwajibika, Sijawahi kuwa na VIDEO kama hyo wala katika kipindi changu chote cha Mahusiano na Nandy hata na Ex Wangu Wengine sijawahi kudeal na Camera Faragha….Nimekwazika Sana,Naomba Radhi Wazazi na Familia Yangu, Ndugu zangu na Mpenzi wangu,Pia Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Sananaa la Taifa,Mamlaka zote Husika, Media na Wadau Wote wa Sanaaa,Management yangu,Mashabiki zangu na Hata watoto na Familia Yangu itakayokuja kukutana na Fedhea hii !nikotayari uchunguzi ufanyike kubaini chanzo cha VIDEO Hii…..Naona sim ni Nyingi lakini siko kwenye hali nzuri hata kidogo naaamini hayo nilioyaaandika atatisha kwa sasa…. “