Huduma za Mabasi ya Mwendokasi zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri ya leo kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi
Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara – Morroco, Kimara – Magomeni Mapipa, na Gerezani – Muhimbili
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), imesema huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa.