Sarah Atulie Tu Harmonize Apindui Kwangu - WolperSTAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper baada ya kudaiwa ‘kumendea’ penzi la mwanamuziki Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ na mpenzi wake Sarah, staa huyo ameibuka na kusema Harmonize hapindui kwake hivyo mpenzi wake huyo ajipange tu.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wolper alisema kuwa ameshangazwa na habari ambayo aliiweka Sarah kwenye ukurasa wake wa Instagram uliokuwa ukionesha kuwa, Wolper alimtumia ujumbe Harmonize kupitia Instagram akieleza kwamba anamkumbuka, kitu ambacho hawezi kukifanya.
“Ninachoona mimi Sarah hajiamini kabisa, siwezi kufanya upuuzi huo kabisa, yeye yupo na mwanaume lakini bado anahangaika mitandaoni, hajui kuwa mwanaume wake hapindui kwangu hata siku moja, akae ajitulize tu zamu yake ya kulia bado haijafika,” alisema Wolper.