Wakati homa ya pambano la watani wa jadi ikiendelea kushika kasi, tayari viingilio vya mchezo huo vimeshatajwa.

Selcom ambao ni waandaji wa tiketi za michezo ya ligi kuu, wametaja viingilio vya mchezo huo utakaopigwa Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio hivyo ni Tshs 30,000 kwa VIP A, VIP B na C ni 20, 000 huku Mzunguko ikiwa ni 7000 tu.

Tayari Selcom wameshaanza kuuza tiketi hizo ambazo ni za mfumo wa kielektroniki.