WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)January Makamba amesema serikali imefanikiwa kudhibiti matukio ya uvuviharamu kwa zaidi ya asilimia 80 katika maeneo ya bahari na maziwa baada ya kuimarisha doria na ukaguzi wa samaki wanaovuliwa.

Aliyasemahayo wakati wa upandaji wa mikoko katika Pwani ya Bahari ya Hindi ambayo
ilipandwa eneo la Mwambani Jijini Tanga chini ya Udhamini wa Mfuko wa
Vodacom (Vodacom Faundation).

Alisema kuimarika kwa doria hizokumesaidia wananachi kuwa na uelewa mpana kuhusu madhara ya uvuvi haramuna hivyo kuanz kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo ikiwemo ulinzi wa
mazingira ya bahari ya hindi na rasilimali zake.

Waziri huyoalisema pamoja na jitihada za wizara katika kudhibiti fukwe za bahari
zinasiendelee kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi lakini bado kuna
maeneo mengi ambayo yanahitaji kuhifadhiwa kwa kupandwa miti ya mikoko.

Pamoja na hayo Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuruVodacom Foundation kwa kuja na kampeni ya upandaji wa mikoko ilikuhifadhi mazingira ya bahari kwa kile alichosema kuwa kutasaidiakuboresha mazingira hayo.

Naye kwa upande wake Mwakilishi waVodacom Foundation Rosalynn Mworia alisema taasisi hiyo kwa kushirikianana chama cha skauti Tanzania waliamua kuja na kampeni hiyo upandaji wa mikoko ili kuhifadhi mazingira ya Fukwe.

Alisema kwamba kwakuanzia kampeni hiyo wameanzia kwa mkoa wa Tanga na wanatarajia
kuipeleka nchi nzima ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira nakukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.