The Art Of “MAISHA FAINALI NI UZEENI” niliporudi fresh from USA niliwaomba TFF wanipe ruhusa niwasaidie kutengeneza mfuko maalum wa kuwasaidia Wachezaji wa soka wanapoacha kucheza soka nikawapa mfano mdogo wa Mchezaji maarufu wa “AMERICAN FOOTBALL” OJ Simpson yeye alicheza mpira kwa Miaka 15 ambayo kila mwaka alikua anakatwa 10% ya mshahara wake na Chama cha NFL ambacho Sheria ya USA inawapa nafasi ya kuchagua biashara yenye faida na kuwekeza huko siku OJ alipostaafu akaanza kulipwa $25K kwa mwezi mpaka leo ambazo ni faida kutoka zile 10% alizokuwa anakatwa kila Mwaka kwenye mshahara wake ..nikawaambia sio TFF tu bali hata Wasanii wanatakiwa kuanza kufanya hayo mambo.ya kukatwa 10% ya mapato yao kwa Mwaka ili ziwe invested kwa miaka kama 20 at a Fixed Account huku zikitumika kuwekeza kwenye biashara kama za Sigara na Beer au Petroli kwa mujibu wa Sheria kusudi mbele ya safari ziweze kuwasidia Uzeeni au Wanapostaafu …juzi nilienda kumuona Mzee Majuto Hospitalini inasikitisha sana kwamba ni hivi karibuni tulikua tunaaminishwa kwamba ana mali nyingi sana kumbe sio kweli and then linakuja swali la msingi je makampuni yote aliyowahi kufanya nao kazi yamemdhulumu? ni swali ambalo wengi tunajaribu sana kujiridhisha na majibu rahisi sana kuwa ni kweli cause tunaweza kwenda kwenye mikataba tukakuta kwamba kila kitu kilifanyika kama inavyotakiwa…guys kupigania maisha mazuri bila kufikiria mbele ya safari yaani uzeeni ni kazi bure halafu nimeona kila haya matatizo yanapotokea tunawarushia lawama Serkali na wengine lakini sio wahusika wenyewe guys tujifunze kuwa responsible siwezi kumlaumu sana Mzee Majuto he is an old timer huenda hajui kabisa mambo ya kuwekeza for future but vipi Viongozi wa vyama vya Wasanii? ambao kila Sherehe kubwa zinapofanyika hukaa mbele meza kuu na kutambulishwa kwa mbwembwe nyingi sana huko kwenye hivyo vyama huwa wanafanya kazi gani haswa? .ninaomba kuwakumbusha Wasanii na Wachezaji wa Soka Tanzania kwamba tunatakiwa kujifunza kutoka kwa waliotutangulia haiewezekani kila Mwaka haya mambo ya Mchezaji au Msanii kushindwa uzeeeni au baada ya kustaafu yanayotokea na yakaendelea kujirudia rudia TUBADILIKE! – @lemutuz_supebrand