Mchekeshaji Emmanuel Mathias maaarufu kama Mc Pilipili ameonyesha maumivu aliyoyapata baada ya kuona aliyekuwa mpenzi wake Nicole Franklyn kuolewa na mwanaume mwingine na kufanywa kuwa Mc katika harusi hiyo.

Mc Pilipili ameyaandika maumivu hayo kupitia instagram account yake kitendo ambacho hakijazoeleka na mashabiki kwa mchekeshaji huyo kuandika maumivu kupitia ukurasa wake wa instagram.

“huyu ni wewe ukinivua koti nilipotoka kuchekesha ukiwa umevaa jezi yangu ya SIMBA MABINGWA Kweli ndo umeamua kuolewa na huyo @mwijaku ambae mimi hanigusi kwa lolote!!??? wigi lako bado liko nyumbani hilo ulilovaa hapo na iyo kanga yako ipo pia USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO….UTAJANIKUMBUKA!!