Klabu Timu ya Yanga imeshinwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwenye michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, baada ya kutoka sare tasa ya bila kufungana na Rayon Sports ya Rwanda.
Kwa Matokeo hayo Yanga sasa inaburuza Mkia katika Kundi lao la D ikifikisha point moja .
Matokeo ya mechi nyingine Gor Mahia ya Kenya imetoka sare ya 0-0 na USM Alger .
Mechi inayofuata Yanga itacheza na Gor Mahia ya Kenya.

Katika Kundi la Yanga msimamo uko kama ifuatavyo….. Rayon Sports ina Pont 2, Gor Mahia ina point 2, na Alger ina Point 4