MUIGIZAJI wa Bongo Muvi, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa hata kama hajapata bahati ya kukaa na mume muda mrefu kama mke lakini kumemfunza kujua maisha mbalimbali na kuwa shupavu kwa mapito aliyopitia.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu, Davina alisema Mungu amemjalia kupitia kwenye ndoa mbili lakini hakubahatika kukaa kwa muda mrefu lakini kikubwa ni kwamba ndoa hizo zimemfunza mambo mengi sana ya kujituma ili aweze kuwalea watoto wake vizuri.

“Siwezi kujilaumu hata siku moja kwa nini sikai kwenye ndoa zote nilizozipitia bali ninachojua ni kwamba zimenifundisha mambo mengi sana hasa ya kujisimamia mimi kama mimi na kuendesha familia nikiwa kama mwanamke mwenyewe bila mtu mwingine pembeni,” alisema Davina.