MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Mwanaheri Ahmed amesema kuwa japokuwa ameingia kwenye ndoa hivi karibuni lakini hana parapara ya kupata mtoto kwanza mpaka afurahie maisha ya ndoa kidogo na mumewe ndipo anaweza kuzaa.

Msanii huyo alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na Amani ambapo alisema, kama mwanamke anajua ni wajibu wake kuzaa ila ndugu na jamaa watamsamehe kwa sasa mpaka baada ya miaka miwili.

“Napenda sana mtoto lakini najua tu nikizaa mapema mapenzi yote nitayahamishia kwa mtoto wangu sasa ni bora mimi na mume wangu tupeane raha kwanza kisha mambo ya mtoto baadaye kidogo,” alisema Mwanaheri.