Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume.

IGP Sirro amekutana na Fatma aliyefika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kujitambulisha tangu alipochaguliwa kuongoza Chama hicho ambapo pia walijadiliana masuala kadhaa ya kisheria.