Director wa video za muziki Bongo, Nisher ametaja video tano za muziki ambazo kwa upande wake zinafanya vizuri.

Nisher ametaja video hizo ni Wayu Wayu ya Dogo Janja ambao ameiongoza yeye, Papa ya Gigy Money iliyoongozwa na Lucca Swahili, Sitamani ya Mimi Mars na Chapaa ya Tammy The Baddest ambazo zote zimeongozwa na Joowzey.

“Video yoyote ya sasa hivi, ya hivi karibu kutoka kwa Travellah ni kali,” Nisher ameiambia Bongo5.

Nisher kwa sasa anatamba na video ya Lulu Diva inayokwenda kwa jina la Homa ambayo ameiongoza yeye. Video hiyo ilitoka April 13, 2018.