STAA wa filamu ambaye kwa sasa amegeukia Muziki wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameapa lazima naye aolewe na mwanaume kutoka nje ya nchi kama alivyofanya msanii mwenzake, Alikiba.

 Sabby ambaye aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano na Alikiba kabla ya kufunga ndoa na Amina Khalef huko Mombasa, Kenya alisema, siyo kwamba anaumia Kiba kufunga ndoa nje ya nchi lakini kwa mtazamo wake ameona wanaume wengi Bongo wababaishaji tu.

“Yaani lazima nilipe hili, alichokifanya Kiba ni sawa lakini na mimi kama msanii naangalia hukohuko, lazima nitaolewa nje ya nchi sitaki Bongo wababaishaji wengi, wana maneno ya mdomoni tu vitendo hakuna,” alisema Sabby anayedaiwa kuhamishia maisha nchini Kenya. Sabby alishawahi kuolewa mara mbili lakini ndoa zake zote hazikudumu zaidi ya mwezi.