The Art of Overpaying jana nilikigusa Chama cha Soka Tanzania kuhusu habari za Kiongozi wake mmoja kulipwa Mshahara wa Tsh. 7M kwa mwezi kuwa ni Mshahara ambao haufanani na matokeo ya soka nchini na pia ni Mshahara ambao haufanani na hali halisi ya mapato ya Soka hapa nchini na kama kawaida yao washabiki wa soka nchini nimeona kuna mapovu mengi sana ya kawaida ya kujifanya wao huko kwenye Soka wanajua sana sisi wengine wote tusiojihusisha huko hatujui kitu na kuna mpaka waliokwenda mbali na kujifanya eti hizo ni pesa toka FIFA …binafsi simjui yoyote huko TFF that nina Chuki au Wivu hapana ila nimeona majuzi mchezaji wa zamani maarufu Modesta akihangaika kukosa matibabu kwa kukosa Bima ya Afya then nikajiuliza inawezekana vipi mchezaji hana Bima ya Afya lakini Kiongozi wa Chama chake cha Soka analipwa Tsh. 7M kwa mwezi?…halafu ninaambiwa kwamba huko TFF kuna mpaka Kiongozi anayelipwa USD $ 20K Per Month now kama hizi hbari ni za ukweli then ninasema bila kupepesa macho kwamba TFF bado ni Shamba la Bibi HAIWEZEKANI kwa mazingira magumu tunayoyasikia kila siku kuhusu gharama za uendeshaji wa soka nchini halafu huko kuwe na watu wanaolipwa mapesa ya ajabu hivi huku wachezaji wa ligi ya TFF wakiteseka na kucheza katika mazingira magumu sana ninasema it is wrong na Serikali inapaswa kuingilia kati na kuhakikisha wanarekebisha mazingira haya ya TFF kulipana mishahara ambayo hailingani na uhalisia wa Soka nchini ….tumepumbazwa kwa muda mrefu sana kwamba Soka nchini linahusu FIFA au CAF zaidi huu ni uhuni wa ajabu sana ambao umesababisha pesa za Soka Tanzania kuhujumiwa sana na kwa muda mrefu sana mpaka majuzi Serikali ya Awamu ya Tano ilipoamua kuingilia kati ….ninarudia tena ni Aibu kwa Mtanzania yoyote leo kulipwa Tsh. 7M kwa mwezi eti kuongoza TFF chama chenye madeni kila kona na kinachodaiwa malimbikizo ya kodi kila wakati na Serikali …hizi nonsense za eti wanapewa pesa na FIFA za kujilipa mishahara ni uzushi tu wa kitoto na ni unacceptable…ni matumaini yangu kuwa baada ya hizi habari Serikali itawatupia macho huko TFF na kuhakikisha kunakuwa na Mishahara inayoendana na uhalisia wa ubora na mapato ya soka nchini! – @lemutuz_superbrand

SHARE
Previous article
Next article