Bill Nass amesema kuwa anaamua kuoa kutokana anapenda familia, pia wasanii wanatakiwa kuwa kama watu wengine kwani kufanya hivyo haimaanishi msanii atashuka kimuziki.

“Niliposti kuhusu kuoa na pia kuhusu nani nitamuoa nitaamua mimi sio mtu mwingine. Mtu kama Alikiba anaweza kuoa na game yake bado ipo strong kuna kila haja, na pia inatambulisha kwamba ndoa ni jambo muhimu lakini pia sisi ni wasanii na ni watu kama wengine,” Bill Nass ameiambia Wasafi TV.

Ameongeza kuwa pindi alipoenda katika harusi ya Alikiba aliguswa na jinsi mtoto wa muimbaji huyo alivyotaka kusoma dua.

“Mtoto wake alikuwa happy sana kwenye ile harusi kwa hiyo ile ilini-impress zaidi,” amesema.