Kipa wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Sergio Romero ameondolewa katika kikosi cha wachezaji 23 waliochaguliwa kwa ajili ya michuano ya Fainali za kombe la Dunia 2018 Nchini Urusi baada ya kuumia goti (Knee Injury).

Argentina wamebakiwa na Magolikipa wawili sasa Willy Caballero anayekipiga katika klabu ya Chelsea na Franco Armani anayekipiga River Plate.