Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Tulia Ackson akitambulisha wageni wa jukwaa la Spika wakati wa kikao cha thelathini na tano cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma


Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza umoja huo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini ambapo atatumikia kwa muda wa miaka mitatu


Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe.Stephen Maselle akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza Bunge hilo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini


Wanafunzi wa Sekondari ya Huruma ya Jijini Dodoma(kushoto) na Wanachuo wa Chuo cha Diplomasia(kulia) wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga na Naibu wake Mhe.Dkt.Suzan Kolimba wakipitia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kabla ya kuwasilisha leo Jijini Dodoma


Mbunge wa Viti Maalum Mhe.fatma Toufiq(CCM) akiuliza swali kutaka kujua mpango wa Serikali kudhibiti hali ya wanafunzi kupewa ujauzito na waendesha bodaboda leo Jijini Dodoma