Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief ameahidi ataachia wimbo wake wa mwisho uitwao ‘Saratani’ kueleza namna muziki ulivyomtafuna na kumwaribia maisha yake.

Muimbaji huyo amesema hayo wiki hii wakati akizungumza na Bongo5 kuhusu kauli yake ya kuachana na muziki na kufanya shughuli nyingine nje ya muiziki.

“Siwezi kuwaacha watu hivi hivi, ngoma yangu mpya inaitwa Saratani, nadhani watu wanajua maana ya Saratani kitu ambacho kinakula ndani kwa ndani,” alisema Q Chief.

Aliongeza, “Huu ni mwimbo ambao nautoa, utakuwa wimbo wa mwisho, watu wajaribu kutofautisha kiki na maisha halisi ya mtu, kiki ni ile unanunua magari unapost na kuonyesha ufahari, halafu maisha ya mtu ni haya. kwahiyo huu utakuwa ni wimbo wangu wa mwisho”

Muimbaji huyo alidai anaacha muziki baada ya kufanya kazi nyingi bila kuwa na mafanikio yoyote katika maisha yake.