Msanii wa muziki wa kizazi kipya Billnass amesema kuwa mwanadada aliyewahi kuwa nae katika mahusaiano ya kimapenzi Nandy ni kama dada yake kwakuwa uhusiano wao uliisha kitambo.

Billnass amefunguka hayo  ambapo amesema kuwa hawezi kumuita mwanadada huyo ‘Ex’ wake kwakuwa waliachana kitambo na mahusiano yake hayakudumu muda mrefu.

“Nandy ni dada yangu kibusara siwezi kumuita ‘Ex’ wangu kwakuwa nilivyoachana nae nimeingia kwenye mahusiano na wasichana wawili tofauti hivyo historia hiyo imekuwa ya zamani sana”.

Ameendelea kusema kuwa jina hilo ameliona kuwa ndio lenye heshima zaidi kwa wakati huu, msikilize hapo chini Billnas akifunguka zaidi