Mwanadada kutoka kiwanda cha Bongo movies, Shamsa Ford ambaye ameolewa na mfanyabiashara Chidi Mapenzi amesema kuwa hajamfilisi mume wake bali amebadilisha maisha yake.

Shamsa amesema hayo  kuwa mume wake hajafulia kama watu wanavyosema bali amemsaidia kupunguza maisha ya ujana aliyokuwa nayo awali.

“Mimi huwa napenda kuishi maisha halisi huwa sipendi shobo na nilifanikiwa kumbadilisha mume wangu kwa kumshauri kuachana na baadhi ya vitu vya ujana na sasa hivi anafanya vitu kama mume wa mtu na mwenye majukumu wala hajafulia ila kapunguza matumizi yasiyo ya lazima amekuwa mtu mzima”. Amesema Shamsa

Shamsa ameongeza kuwa wanaosema amefulia wanakosea maana wao wameamua kuishi maisha yao ambayo watu hawawezi kuwaelewa,msikilize hapo chini amefunguka zaidi.